Resumen del episodio
Afrika imezindua rasmi Wakala wa Ukadiriaji wa Mikopo wa Afrika, Africa Credit Rating Agency (AfCRA), hatua inayolenga kushughulikia changamoto za gharama kubwa za mikopo na kuvutia uwekezaji zaidi kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Je, kuanzishwa kwake kutapunguza kweli gharama za mikopo kwa mataifa ya Afrika, au ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mageuzi ya kifedha?
Afrika imezindua rasmi Wakala wa Ukadiriaji wa Mikopo wa Afrika, Africa Credit Rating Agency (AfCRA), hatua inayolenga kushughulikia changamoto za gharama kubwa za mikopo na kuvutia uwekezaji zaidi kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Je, kuanzishwa kwake kutapunguza kweli gharama za mikopo kwa mataifa ya Afrika, au ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mageuzi ya kifedha?
Episodios
Afrika kuzindua taasisi ya ukadiriaji mikopo, je itasaidia?
EscuchadoAfrika imezindua rasmi Wakala wa Ukadiriaji wa Mikopo wa Afrika, Africa Credit Rating Agency (AfCRA), hatua inayolenga kushughulikia changamoto za gharama kubwa za mikopo na kuvutia uwekezaji zaidi kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Je, kuanzishwa kwake kutapunguza kweli gharama za mikopo kwa mataifa ya Afrika, au ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mageuzi ya kifedha?
Je, Afrika itapata sauti inayodai katika uchumi wa dunia?
EscuchadoKwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na gharama za juu za kukopa katika masoko ya kimataifa. Fedha nyingi ambazo zingetumika katika afya, elimu, miundombinu na ajira zinaishia katika kuhudumia madeni, hali inayoweka shinikizo zaidi kwa uchumi wa nchi hizi. Je, hitaji la Afrika la kuwa na mfumo mpya wa kifedha duniani wenye uwakilishi na usawa zaidi litawezekana?
Kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu: mwanzo wa mapinduzi ya nishati Afrika Mashariki?
EscuchadoKenya inaagiza karibu mahitaji yake yote ya bidhaa za Petroli kutoka nje, hii ikiwa na maana kuwa bei na upatikanaji wa mafuta katika nchi hii, na kwa kiasi kikubwa katika ukanda unaweza kuathiriwa na mambo yanayotokea katika masoko ya kimataifa, hata hivyo habari njema ni kuwa bilionea wa Afrika Aliko Dangote anajenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu. Kwanini hatua hii ni muhimu? Tufuatilie
Hormuz na Bab el-Mandeb: Njia za baharini zinazotikisa uchumi wa dunia.
EscuchadoMsikilizaji hebu fikiria mafuta unayoweka kwenye gari lako, bidhaa zinazofika kwenye maduka yetu kutoka Asia, mbolea inayotumika kwenye kilimo, au hata gharama ya kusafirisha kahawa na chai kutoka Afrika kwenda masoko ya nje, kwa namna moja au nyingine, sehemu ya uchumi huu inategemea bahari na kufungwa kwa njia ya Hormuz na sasa ile ya Bab el-Mandeb kunauweka uchumi wa dunia hatarini. Ungana nami kwenye makala ya wiki hii kufahamu zaidi.
Maisha mapya: Jinsi akina mama vijana wanavyobadilisha ujuzi kuwa fursa
EscuchadoNchini Kenya, suala la mimba za utotoni ni changamoto. Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya taofa nchini Kenya kupitia utafiti wa mwaka 2022 asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 walikuwa wamewahi kupata ujauzito. Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii, tunaangazia namna akina mama hawa wanavyogeuza ujuzi, juhudi na fursa za kiuchumi kuwa njia ya kujitegemea na kuwajengea watoto wao maisha yenye matumaini zaidi.